Visa vya maambukizi ya ugonjwa wa coronavirus vyapanda hadi 110 Kenya

Idadi ya visa vya ugonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imefikia 110 baada ya visa vingine 29 kuthibitishwa.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari jijini Nairobi waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba watu wengine wawili wamepoteza maisha yao kutokana na maambukizi ya virusi hivyo.

Idadi hiyo inaongeza idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia 3. Amesema kwamba wagonjwa waliofariki wanatoka miji ya Nairobi na Mombasa.

Waziri huyo pia amepiga marufuku usafiri wa Wakenya kuelekea katika maeneo ya mashambani akionya kwamba huenda wakapeleka maambukizi ya virusi hivyo katika maeneo hayo.


Faith Evans

1 Blog posts

Comments
alvin 11 months ago

Pandemic